Tuesday, 10 December 2013

Kikwete- tumuenzi Mandela kwa kuacha kilipiza kisasi!!

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuacha tabia ya kuwa roho ya mlipiza kisasi badala yake wawe watu wa kusamehe na kusahau kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi moja kwa moja Rais mstaafu wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela.
Rais Kikwete ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia maelfu ya watu waliojitokeza kwenye sherehe za kutimiza miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe zilizofanyika katika uwanja Taifa.

Rais Kikwete ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia maelfu ya watu waliojitokeza kwenye sherehe za kutimiza miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe zilizofanyika katika uwanja Taifa. 


Rais Kikwete amesema mara baada ya Rais Mandela kutolewa gerezani  hofu ilitawala Afrika ya Kusini, watu wengi wakitambua kuwa atakapochaguliwa kuwa Rais badala ya kuijenga nchi ataanza kulipiza visasi kwa wale wote waliotumika kwa namna moja ama nyingine kumtesa yeye na watu wa nchi yake.

Akimtolea mfano Hayati Mandela, Rais Kikwete alisema “badala yeke Mzee Mandela alitoa tamko la kuwasamehe wote waliohusika kuwabagua watu wa Afrika ya Kusini, na kisha aliunda tume maalumu ya maridhiano ili kujenga umoja kati ya watu wenye ngozi nyeupe na wenye ngozi nyeusi, jambo hili ni la ajabu sana” amesema Kikwete.

“Hiki ni kipimo kikubwa cha ukomavu wa kisiasa, yatupasa watanzania na viongozi mbalimbali kuenzi jambo hili la kusameheana na kutokuwa walipiza visasi, hapa tulipo wengine wanasema kabisa nikichaguliwa watanikoma….. lakini nawasihi tumuenzi Mzee Mandela kwa kuiga mambo mema aliyoyafanya ambayo hadi hivi leo yamechangia kukuza uchumi wa Afrika ya Kusini, “Amesema Kikwete.

Amesema Tokea enzi za Tanu Tanzania imekuwa karibu sana na vyama vya ukombozi wa mataifa mengi Afrika, kikiwemo chama chas ANC ambacho kilikuwa kikiongozwa na Marehemu Mzee Mandela, hivyo aliwasihi watanzania waendeleze umoja huo .

“Kuna jambo moja ambalo hamlijui mwaka wa 1964 Mzee Mandela alikuja nchini na kufikia kwa mweka hazina wa Tanu, Siro Swai, alikuwa akielekea kwenye mafunzo ya kijeshi Algeria, aliacha buti zake za kijeshi akieleza kuwa atakaporudi atakuja kuzichukua lakini haikuwa hivyo, nilipokuwa waziri wa mambo ya nje, mke wa swai alinifuata na kunieleza, nasi tulilazimika kuzirudisha kipindi hicho ambacho Mzee Mandela alikuwa Rais wa nchi hiyo tayari,” Anaeleza Kikwete

No comments:

Post a Comment