Spika wa bunge 11, Mhe Job Ndugai(mbunge wa Kongwa)
Chama Cha Mapinduzi tawi la Moscow-Urusi tunayo furaha kubwa kupokea ushindi uliotukuka wa Mhe Job Ndugai kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la 11 la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Uongozi wa tawi unapenda kuchukua fursa hii ya kipekee kuwashukuru wabunge wa CCM kwa kuungana kwa pamoja, kuwa na imani na kumpigia kura nyingi Mhe Job Ndugai, ushindi wa Mhe Ndugai ni ushindi wa watanzania kwani Mhe Ndugai ni kiongozi jasiri, mwadilifu,mchapakazi, anayependa watu na anayependwa na watu hivyo tunaamini atawatendea haki watanzania kupitia muhimili huo muhimu wa serikali.
Katika taarifa yake fupi, mwenyekiti wa tawi Ndg Salim Mfungahema alisema anafahamu vizuri pasi na mashaka utendaji na uwajibikaji ulio bora wa Mhe Ndugai kwani aliwahi kufanyanae kazi ya kuimarisha chama katika jimbo la Kongwa mwaka 2012. Kupitia ziara iyo ya wiki moja jimboni kongwa Ndg Mfungahema anasema alijifunza mambo mengi kupitia mwanasiasa huyo mkongwe na anayekubalika sana jimboni kwake, hivyo anaamini CCM imefanya chaguo sahihi na tunaamini ataongoza vema muhimili huo wa kutunga sheria na kusimamia serikali.
Kidumu Chama Chama Mapinduzi,
Imetolewa na katibu wa tawi,
Ndg Hassan Kapilima.
Trh 17.11.2015.









