Rais wa awamu ya tano Dkt John P Magufuli
Leo tarehe 5 mwezi wa 11, 2015. Tanzania imeandika historia nyingine mpya kwa kupata Rais mpya wa awamu ya tano.
Chama Cha Mapinduzi tawi la CCM Moscow Urusi tunayo furaha kubwa kushuhudia jinsi raisi wa awamu ya nne na rais wa awamu ya tano walivyoweza kubadilishana madaraka katika misingi ya amani, upendo na kuheshimu katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, aidha uongozi wa tawi tunajivunia taswira ya kipekee ya mfumo wa uongozi ndani ya taifa letu, misingi ambayo imejengwa kikamilifu na TANU na ASP, na badae CCM.
Rais Mhe, Dkt John Pombe Magufuli akila kiapo
Uongozi unapenda kuchukua fursa hii ya kipekee kumpongeza rais wa awamu ya tano Dtk John P Magufuli kwa kula kiapo cha uaminifu, uadilifu, kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Mbali na pongezi hizo uongozi unaamini rais wa awamu ya tano ni mchapa kazi, mwadilifu, kiongozi hodali na mwenye msimamo thabiti, hivyo tunaamini ndoto za watanzania zitatimia, kwa kufanya hivyo atakuwa amewatendea haki watanzania, pia atakuwa amekipa heshima chama chake CCM na kukihakikishia ushindi daima.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
IMETOLEWA NA MWENYEKITI WA TAWI.
SALIM .A. MFUNGAHEMA

No comments:
Post a Comment