Chama cha mapinduzi tawi la CCM-Moscow Urusi tumepokea kwa furaha kubwa ushindi wa CCM katika nafasi mbalimbali, Urais, ubunge na udiwani.
Aidha Uongozi wa CCM Moscow unapenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kumpongeza rais mteule wa awamu ya 5 wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwakuchaguliwa na watanzania kwa kura nyingi zilizompa ushindi mkubwa na kukipatia chama cha mapinduzi ushindi kishindo, aidha ushindi wa Dr Magufuli umedhihirisha wazi CCM ni chama bora, imara chenye nguvu na ni chama ambacho ilani yake inatekelezeka.
Pia tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa rais anayemaliza muda wake Dr Jakaya Kikwete kwa kumaliza muda wake wa kuliongoza taifa la Tanzania miaka 10, kwa mafanikio makubwa na iyo ndio siri ya ushindi wa CCM.
Pongezi nyingi ziwaendee marais wastaafu mzee Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, wanachama wa CCM, na watanzania wote kwa ujumla bila kujali itikadi ya vyama vyao, kwa kuendelea kuwa na imani na CCM, kuichagua na kuipa ridhaa ya kuongoza dola.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki CCM Daima.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Imetolewa na mwenyekiti wa tawi ndg Salim A. Mfungahema

No comments:
Post a Comment