Uongozi wa tawi la CCM-Moscow-Urusi umepokea kwa furaha uteuzi wa Dr Asharose Migiro kuwa Mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, katika taarifa yake mwenyekiti wa tawi la CCM Moscow Urusi Ndg Mfungahema Salim alisema huu ni mwendelezo wa rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kuonyesha umakini wake katika kuteua viongozi makini ambao wanaweza kupeperusha bendera ya CCM na kutoa mchango mkubwa kwa chama na serikali.
M wenyekiti wa tawi la CCM-Moscow Urusi Ndg Salim Amani Mfungahema
Hapo awali bwana Mfungahema aliandika makala inayoelezea kwa ufupi wasifu wa Dr Asharose Migiro na umakini wa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete katika maeneo ya utawala bora, uchapakazi na hasa katika kipengele cha uteuzi wa wasaidizi wake. Nikweli kwamba Dr Asharose Migiro amekuwa ni mwanasiasa mwenye mvuto mkubwa katika siasa za Tanzania, tunamshukuru Rais kwa kuwa msikivu na kuangalia watendaji wenye kipaji na hasa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

KATIBU WA CCM-USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA MBUNGE WA HESHIMA MTEULE DR ASHAROSE MIGIRO
Uteuzi huo unamrejesha Dk Migiro bungeni baada ya kuondoka Januari 5, 2007 akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na kuhudumu hadi alipomaliza muda wake Januari mwaka jana.
Baada ya kurejea nchini, Dk Migiro aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais jana, ilimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka akisema uteuzi huo umeanza tangu juzi.
Uteuzi huo unatokana na mamlaka ya kikatiba aliyo nayo Rais Kikwete ya kuteua wabunge 10.Mwanasiasa huyo aliyezaliwa Julai 9, 1956, aliwahi pia kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.
IMETOLEWA NA OFISI YA KATIBU MKUU WA TAWI LA CCM-MOSCOW
KATIBU WA TAWI, NDG HASSAN KAPILIMA

No comments:
Post a Comment