Sunday, 8 December 2013

KATIBU MKUU WA CCM MH KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO, MAPOKEZI MAKUBWA YAMSUBIRI DAR ES SALAAM.



CHAMA  Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dar e s salaam, leo jumapili  kimeandaa mapokezi makubwa 
ya Katibu Mkuu wao, Abralrahaman Kinana , kufuatia kumaliza ziara katika Mikoa mitatu ya Ruvuma, 
Mbeya na Njombe kwa mafanikio makubwa.

Kinana  na ujumbe wake akiwemo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  pamoja na Katibu 
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Migiro  watapokelewa  katika Stesheni ya Tazara  jioni .

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar e s salaam, Juma  Simba  amewambia waandishi wa habari 
kuwa katika mapokezi hayo kutakuwa na Burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali wa muziki wa Kizazi Kipya.

Kutokana na mapokezi hayo, CCM imetoa wito kwa Wananchi pamoja na wana-CCM kujitokeza kwa 
wingi katika mapokezi hayo.

Katika Mikoa ambayo Katibu Mkuu wa CCM, ameweza kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili 
wananchi na kuzitolea ufafanuzi ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza mawaziri husika kutokaa ofisini na 
badala yake weende vijijini kuwasikiliza wananchi.

UHURU  FM-DSM

No comments:

Post a Comment