Kwa mujibu wa Waziri Membe, kubaguliwa kwa Tanzania katika ushirikiano wa Afrika Mashariki kumeegemea katika mambo makuu matatu ikiwepo kupeleka askari kupigania amani nchini Congo dhidi ya waasi wa M23,pia kitendo cha Tanzania kukataa ardhi kuwa sehemu ya mali ya Afrika Mashariki huenda pia imepelekea mchango mkubwa kwenye choko choko hizo. Na tatu alisema kwamba pengine kunamtu alikuwa anataka kuongoza Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC)na ameona Tanzania imekataa.
"Inawezekana hawapendi tupige M23, au wamekasirika kutotoa ardhi kwaajili ya shirikisho,au kuna mtu alikuwa anataka kuongoza na ameona hatujataka lkn ni bora waseme.,"alisema Membe.
Akiongelea suala la ardhi;
Waziri Membe alisema, hauwezi leo ukaitaifisha ardhi ya nchi nyingine na kuviacha vizazi vijavyo bila mali,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa “kwa vyovyote vile, jumuiya hii ya Afrika Mashariki lazima iende kwa taratibu.
Akielezea vitendo vya wakuu wa nchi hizo wananchama zilizojitenga, Membe alisema,"Kama mnatatizo halafu mnakutana nchini inayohusu tu bila kutuhusisha Tanzania kama wanashirikisho na mnatatua, hilo si jambo jema. Eti mkiona jambo linalohusu Uganda basi mnaenda wenyewe na kutatua.Si vyema".
Alisema kuwa pamoja na kuwa, hata kama wakuu wa nchi hizo kuita shirikisho lao kuwa 'The coalition of the willing' yeye ameiita...‘this is the coalition of the fear’.
Ukuangalia laslimali, watu, membership ktk nchi za SADC TZ hatuachiki,tupo mahala ambapo hatuachiki, kwahiyo sioni Tz kwaharakaharaka inaweza kuachiliwa…hata ukiangalia Uganda kuwa wakiweka bidhaa zao na wajaribu kuuziana badoi watataka soko hapa kwetu.
Waziri Membe alisema cha kushangaza ni kwamba majirani zetu wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ambayo ni mfano pekee wa kuigwa kwa uzoefu wa muungano. “Sisi ni taifa na sio muungano wa makabila matatu au manne, asikudanganye mtu katika Afrika Tanzania ndiyo mfano wa pekee wa kuigwa duniani kwa kutambua mambo ya muhimu juu ya Muungano…ona muungano wetu Tanganyika na Zanzibar tumeulea na kuulinda sana,"alisema Waziri huyo.Akiongelea suala la kuwa na sarafu moja.
Waziri Membe alisema,;
...hakuna sasa dunia yenye kutumia sarafu moja, waliotumia sarafu moja wapo katika moto mkubwa sana.
Nasisitiza kuwa suala la kuwa na monetary union lazima uwe uamuzi wa kiuchumi na si political decision huko ni kuingilia uchumi kupitia mambo ya siasa.Na wao wamelichukulia hili pasipo kujali kuwa ni suala la kiuchumi," alisema Membe.
Kuhusu Federation siyo kitu ya kukimbilia, Common Wealth imeruhusu bidhaa kutembea kote katika Afrika mashariki hata watu kuomba kazi na kufanya kazi nchi nyingine ruksa..hiyo ndo characteristic feature ya common market kama bidhaa inaweza kwenda kokote na mambo hayo yote yakaenda pamoja basi sarafu automatically itatumika moja kwa moja yenyewe tu, na si kwa kupanga kwa muundo wanaosema.
“Sisi ndio ‘center of gravity’ na ndio soko kubwa la bidhaa katika ukanda wa Afrika Mashariki - tuna rasilimali zaidi ya majirani zetu, tuna utajiri wa ardhi na bandari nne ambazo ni ufunguo wa kutumia bahari kubwa na kufikia nchi nyingine duniani,” alifafanua Waziri Membe. Bandari hizo ni za Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na bandari ya Bagamoyo ambayo ipo katika ujenzi wa kuifanya iwe bandari kubwa ya kimataifa barani Afrika.
"Tanzania itaendelea kushiriki katika mambo ya kuimarisha amani Afrika kama ilivyo panga haitasitisha, miaka 60 sasa imekuwa ikifanya hivyo, nawakumbusha Watanzania kuwa tabia hii ya nchi yetu katika kushiriki kikamilifu kwa kuwatuma askari wetu kujitolea kutatua migogoro Afrika imeleata medani kubwa ktk nchi za afrika, ni sisi tumekuwa na moyo kuona Afrika na nchi zake zikiwa ktk amani tuna sifa ya kusaidia na kutatua mgogoro in a katika bara hili.
Akiongea juu kupeleka askari Congo na Darfur Membe alisema;
Linapotokea kama Darfur na DRC wangekata tama, sisi ni taifa tunajitoa, huwezi kukuta Watanzania wakilalamika ila tunahesabu kuwa wale askari wetu wamekufa kishujaa, hii ndiyo chachu ya mataifa mengine kufanya kwa moyo ..hao wa upande wa pili waliopoteza watu zaidi, ni siri yao,inapotokea mauaji ya askari mmoja wetu huo upande mwingine ni balaa.
Lakini pamoja na hayo, unakuta bado askari wanataka kwenda kuziba pengo hii ni chachu katika kuleta amani…kupoteza askari inauma lakini pia inawauma hata Ulaya,Umoja wa Mataifa na Afrika ya Kusini wanatoa rambirambi na kuomboleza nasi huku wakisifu ushujaa wa askari wetu.
Sisi na nchi za SADC tulikubaliana kuwa tuunde kikosi kitakachopata ruksa kisheria toka Umoja wa Mataifa kupata chapter mandate ili kupitia sheria basi tushirikiane kuleta amani Congo ambapo tumeshiriki kikamilifu.
Aidha Waziri Membe amewaambia Watanzania kuwa, “wakae wakijua kwamba akufuzae hakwambii toka, utaona tuu mambo yanabadilika.”
“Huu ni muungano wa watu wenye woga,” alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika mnamo mwaka 1977.
“Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika. Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe. Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.
“Jumuiya hiyo ilishawahi kuvunjika na kuungwa tena, na Tanzania hatukuathirika. Tuko tayari kupewa au kutoa talaka, na ikiwezekana labda kutakuwa na talaka rejea,” alisema Waziri Membe. Jumuiya hiyo ya EAC inazijumuisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.
Aidha, Waziri Membe alienda mbali zaidi na kusema kuwa huenda chokochoko ya kutengwa kwetu inatokana na wivu au gere kwa Tanzania kupeleka majeshi yake huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jambo alilosema huenda halijawafurahisha baadhi ya watu katika Jumuiya hiyo.
Taarifa toka kwa Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta.
Taarifa toka kwa Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samuel Sitta.
Tayari Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Samuel Sitta imetoa msimamo bungeni kuhusu kuchukizwa na kitendo hicho, ambacho kinaonyesha wazi kuwa yanayofanyika siyo dalili njema kwa jumuiya hiyo.
Sitta aliliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kadhaa mpaka sasa ikiwamo kutaka ufafanuzi kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba baada ya wiki mbili (yaani tangu juzi) ikishapata majibu itatoa msimamo wake.
Vilevile, Sitta alisema Tanzania haitahudhuria mikutano ya Jumuiya hiyo yenye ajenda ambazo nchi hizo tatu zimekubaliana na kuwa na msimamo wa pamoja, huku ikiwaagiza watendaji wake kutotoa majibu ambayo yatachukuliwa kama msimamo wa nchi.
"Tunachukua fursa hii kutoa msimamo wetu kuwa chokochoko zinazofanyika kuivunja jumuiya hii hatukubaliani nazo, kwani tunaamini kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado ni muhimu kwa wanachi mmoja mmoja, na kwa nchi wanachama," alisema Waziri Sitta.
Tangu nchi ziitenge Tanzania na Burundi, yapo maoni mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na Watanzania ikiwamo kuzishauri nchi zilizobaguliwa kuunda umoja wao ambao utajumuisha nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
CHAMA CHA MAPINDUZI MOSCOW URUSIDK SALIM AMANI MFUNGAHEMA
MWENYEKITI WA TAWI LA CCM-MOSCOW-RUSSIA FEDERATION


No comments:
Post a Comment