Monday, 4 November 2013

PICHA,MKUTANO MKUBWA WA MH:MWIGULU NCHEMBA SHELUI--IRAMBA,AMWAGA DAWATI NA AMBULANCE KITUO CHA AFYA SHELUI

Naibu katibu CCM Tanzania Bara na Mbunge wa Iramba Mgharibi Mh.Mwigulu Nchemba leo jumapili 3/11/2013 amefanya mkutano mkubwa wa hadhara huko  Iramba kata ya Shelui akizungumza na wananchi wake kuhusu shughuli mbalimbali za maendeleo na kukabidhi madawati kwaajili ya shule pamoja na kutoa taarifa ya kununua Ambulance kwaajili ya wana Shelui ya matumizi ya kubebea wagonjwa kituo cha afya cha Shelui.
Mbunge huyo ambaye kwa muda mrefu sasa ameteka media za nchi kutokana na umahili wake wa kisiasa,akiwa amembatana na Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza mambo mengi sana na wanashelui ikiwa pamoja na kuwapa nafasi ya kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali ya mwendeo wa siasa na utekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba amewapongeza sana wakazi na wananchi wa Shelui kwa namna walivyoshiriki kwenye ujenzi wa kituo cha afya ambacho yeye(mwigulu) amechangia mifuko ya cement na mabati.Pia kwa sasa amewanunulia gari la Ambulance kwaajilya wagonjwa,Gari lipo mbioni kuletwa Shelui mapema ndani ya Mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amewaomba Wanashelui kupuuzia kelele zozote za wapinzai za kuhusu yeye,amedai kuwa wapinzani(CHADEMA) wameelekeza nguvu zao kupambana na yeye kwasababu ni tishio kwao na amekuwa mstari wa mbele kufichua maovu wanayofanya na kupanga kuyafanya.Hivyo yeye yupo imara sana na anategemea wananchi wa Shelui hawatatoa nafasi kwa watu waaina hiyo ya CHADEMA.Mwigulu amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwapa nafasi wapinzani nikukaribisha vurugu,uvunjifu wa Amani katika kata yao,Wapinzani ndani ya vyama vyao wanapigana ngumi mwenyekiti kwa mwneyekiti na mmeona namna walivyosababisha kifo cha kijana pale Ndago,walivyomwagia tindikali kijana(Musa Tesha)pale Igunga n.k.alisema Mwigulu.
Vijana endeleeni kujishughulisha na kazi za maendeleo,endeleeni kujikusanya kwaajili ya kutoa misaada ya bodaboda na mikopo kama nilivyofanya kwenye kata zingine,Naomba mshiriki kwenye michezo hasa hii michuano yangu niliyoanzisha.Kukaa bila kazi ni hatari sana kwa kijana ndio maana mnakuja kujiingiza kwenye vyama visivyo na mwelekeo wowote hapa nchini"Mwigulu.
Jambo kubwa la kufurahisha katika Mkutano huu Mh.Mwigulu Nchemba alitoa nafasi kwa wananchi kutoa dukuduku zao,mawazo na maswali ya mambo mbalimbali yanayowakabili.Maswali yote yalijibiwa na mengine kujibiwa na watendaji moja kwa moja,Hatua hii imetoa fursa kwa wananchi kujua mambo mengi hasa matumizi ya mfuko wa jimbo ambapo wengi wao walikuwa hawajui kuwa Mbunge hakutani na fedha ya Mfuko wa jimbo zaidi ya Ofisi ya waziri mkuu na mkurugenzi wa wilaya na kisha kwenda kwa mfumo wa cheki kwenye serikali za vijiji.
Kazi ilikuwa kubwa sana kumuondoa Mh.Mwigulu Nchemba eneo la Mkutano kutokana na umati mkubwa wa wananchi kutaka kumbeba na kusukuma gari lake hadi eneo la barabara iendayo Igunga.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
IMETOLEWA NA KATIBU WA TAWI LA CCM MOSCOW
NDG HASSAN H. KAPILIMA

No comments:

Post a Comment